Psalms 46:1-5

Mungu Yuko Pamoja Nasi

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Mtindo wa alamothi.

1 aMungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2 bKwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa
nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari.
3 cHata kama maji yake yatanguruma na kuumuka,
milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake.

4 dKuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu,
mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi.
5 eMungu yuko katikati yake, hautaanguka,
Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
Copyright information for SwhNEN